Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linamshikilia na linamudu kumhoji Loveliness Daniel Kisile, miaka 30, mkazi wa mtaa Temeke, kata ya Mhandu, wilaya ya Nyamagana, kwa tuhuma za kuiba taarifa za uongo kwa mume wake na ndugu zake kwa ametekwa na watu watatu wa jinsia ya kiume wakitaka fedha ili wasimudu na kuondoa juu zito wake. Taarifa hizo za kweli na zilepelekea kuzua taharuki kwa mume wake, wakwe zake na jamii kwa ujumla.
Tukio hilo limetokea Septemba 24,2025 majira ya 05:30 usiku, huko mtaa wa Temeke, kata ya Mhandu, wilaya ya Nyamagana, ambapo mtuhumiwa Loveness Daniel Kisile, alitoa taarifa ya uongo kwa kumpigia simu mume wake aitwaye Hosea Joel Lusigwa, kwamba ametekwa na watu watatu wa jinsia ya kiume waliokuwa wakitumia usafiri wa pikiki na gari, ambazo namba zake za usajili hakuzitambua, akidai watu hao walimkamata kwa nguvu na kumvisha mfuko wa sulphate usoni kwa lengo la kutowatambua kisha kumpeleka kusikojulikana.
Ambapo, taarifa hizi ziliripotia kituo cha Polisi Nayakato, na mume wa mtuhumiwa akidai mke wake ametekwa na watu wasiojulikana na watekaji hao, wametaka watumiwe fedha kiasi cha shilingi Milioni 10, na wasipotumiwa watamchoma mke wake sindano ya kutoa mimba na baada ya muda mfupi alimjulisha mumewe mimba imetolewa na watoto wake mapacha watatu wamefariki na kumsisitiza atume kiasi hicho cha fedha ili aachiwe huru.
Kwa mujibu wa jeshi la Polisi, upelelezi ulianza mara moja na ilipofika tarehe Septemba 25,2025 10:00 alfajiri askari walifanikiwa kumkamata Loveness Daniel Kisile, aliyekuwa anadai ametekwa huko mtaa wa Mecco, Buzuruga, Ilemela.
Na baada ya mahijiano ya awali mtuhumiwa mtuhumiwa alikiri kutoa taarifa za uongo za kutekwa na kutolewa mimba kama alivyozitoa awali. Pia aliojiwe tena kwa kina juu ya taarifa za kutekwa kama alivyowapatia wakwe na mumewe ambapo aliendelea kukanusha kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote kwa maelezo kuwa amefanya hivyo ili kumdanganya mumewe na wakwe ili waendelee kumuamini na waweze kutoa mahali nyumbani kwao na pesa alizokuwa anadai zitumwe anazihitaji kwa manufaa yake mwenyewe.
Jeshi la Polisi, Mwanza, limetoa onyo kali kwa wananchi kuacha kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya uhalifu hasa yanayohusisha vitendo vya kihalifu vya kutekwa, kudhurumiwa na kufanyiwa ukatili kwa lengo la kuficha ukweli au kujipatia huduma na msaada wa kifedha kutoka kwa watu mbalimbali, kwani yanaleta hofu na taharuki zisizo na msingi katika jamii.
Chanzo: Tanzania Journal