Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi amekanusha taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa warsha ya waamini jimboni humo itafanyika Oktoba 29, siku ambayo ni ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
“Wanaohaingaika wakidhani kwamba Kanisa Katoriki linataka kulumbana au kushindana na serikali hatuna mpango huo.” - Ruwa’ichi
Askofu Ruwa'ichi amesema taarifa hiyo siyo ya kweli na haijatoka ofisi yake na akitaka ipuuzwe, akifafanua kuwa warsha hiyo itafanyika Novemba 29, 2025.
Chanzo: Dw