Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mabasi Mapya ya Mwendokasi Yaongeza Nguvu Kimara - Gerezani

Mabasi ya Kampuni ya Mofat Limited, yaliyopangwa kutumika katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) katika njia ya Gerezani–Mbagala, yameanza rasmi kutoa huduma ya muda ya usafiri katika njia ya Kimara-Gerezani.

Uwepo wa mabasi hayo yanayotumia mfumo wa nishati ya gesi asilia umeleta mabadiliko chanya katika huduma za usafiri kati ya Kimara na Gerezani, kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa abiria katika vituo vya mabasi.

Kituo cha Kimara wilayani Ubungo, ambacho kwa kawaida huzongwa na idadi kubwa ya abiria, leo Oktoba 2, 2025, kimeonekana kuwa na abiria wachache, wakiingia kwenye mabasi kwa utaratibu maalumu wa kupanga mstari.

Hali kama hiyo imeshuhudiwa pia katika vituo vya Korogwe, Kibo, Magomeni hadi Gerezani, ambapo idadi ya abiria imepungua ikilinganishwa na siku za kawaida, hatua inayochangiwa na kuongezeka kwa idadi ya mabasi yanayotoa huduma.

Mwananchi digital leo Oktoba 2, 2025 imeshuhudia mabasi zaidi ya 10 mapya ya Kampuni ya Mofat Limited yakiwa kazini, yakitoa huduma ya usafiri na kuongeza nguvu kwenye mfumo wa mabasi yaendayo haraka (Dart).

Hatua hii imekuja siku moja tu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, kufanya ziara katika kituo cha mabasi cha Kimara na kuwataka wananchi kuwa watulivu na wavumilivu, wakati Serikali ikiendelea kushughulikia changamoto ya usafiri wa mwendokasi, hususan katika kituo hicho.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: