“Changamoto inayotukabili ni rasilimali zetu ni chache, kama mnavyojua mambo mingi tunategemea kupata kutoka nje mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za Kimataifa, mabenki ya Kimataifa lakini yaliyotokea nchini kwetu yametutia doa kidogo, kwahiyo huenda yakatupunguzia sifa ya kupata mikopo kwa urahisi kama tulivyopata muhula wa kwanza wa awamu hii ambao tulikuwa tunapata sana lakini doa tulilojitia huenda likaturudisha nyuma”
“Kwa maana huyo tuna kazi ya kutafuta fedha humu ndani, kutumia rasilimali zetu alizotupa Mungu kuangalia njia gani tutazitumia tupate fedha tukatekeleze miradi , muhula wa pili wa awamu ya sita tutaanza kufanya miradi wenyewe halafu Mashirika yatatuka njiani tutakwenda nao hatutokaa kusubiri tunauza mradi, tunakwenda kubembeleza, mradi unakubaliwa lakini nendeni karekebisheni hili, nendeni yule nenda kam-kiss, huyu usimnyukue lakini yule sijui kamfanyaje, mradi badala ya kupata approval miezi mitatu minne tunachukua mwaka mzima tunabembeleza mradi mmoja mpaka permission inatoka tuna miaka miwili tunamaliza muda wetu hatutosubiri hayo, tutaanza na fedha zetu za ndani” —— Rais Samia baada ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu ya Chamwino Dodoma leo November 18,2025
Chanzo; Millard Ayo