Wanafamilia wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, leo Jumanne (06.01.2026) wamefika nyumbani kwake iliyopo eneo la Ununio jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya maombi maalum na kuchukua baadhi ya mali zake. Wakati huo huo, mama mzazi wa Polepole, Ana Maria Polepole, ameitaka serikali imuachie huru au, endapo anadaiwa kuwa na kosa lolote, imfikishe mbele ya vyombo vya sheria.
“Naomba mwanangu huko aliko wanirudishie. Kama ana makosa ashtakiwe, wamuachie mwanangu nateseka.”
Chanzo; Dw