Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mfanyabiashara Adaiwa Kujinyonga Moshi, Madeni Yatajwa

fanyabiashara katika sekta ya utalii, Azizi Msuya (39), mkazi wa Sambarai wilayani Moshi, amekutwa amefariki dunia akidaiwa kujinyonga nyumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani iliyokuwa imefungwa juu ya kenchi.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi, Oktoba 2, 2025 saa 2 asubuhi katika kata ya Kindi, tarafa ya Kibosho, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, marehemu alikuwa akijihusisha na biashara ya kusafirisha wageni (tours) katika mkoa huo.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa marehemu alijinyonga kutokana na msongo wa mawazo.

Amesema msongo huo ulisababishwa na madeni ya benki na watu binafsi aliyokuwa anakabiliana nayo kwa muda mrefu.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: