Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wanne kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu barabarani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam jana, Jumanne Muliro jana, tukio hilo limetokea jana mchana eneo la Mabwepande, Dar es Salaam.
"Inadaiwa kundi la watu, wengi wao wakiwa wamepanda pikipiki na baadhi wakiwa na mapanga, walifanya vitendo vya unyang'anyi na uporaji huku wakiwa na jeneza la marehemu aliyefahamika kwa jina la Ibrahimu Elia mkazi wa Mabwepande" amesema Kamanda Muliro.
Chanzo; Nipashe