Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Polisi Wawasaka Gwajima, Mnyika, Lema na Wengine 7

Jeshi la Polisi limesema linawatafuta Josephati Gwajima, Godbless Lema, na wengine nane wakiwemo Brenda Rupia, John Mnyika, Machumu Kadutu, Deogratius Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Amaan Golugwa.

Polisi inasema hatua hiyo imekuja kufuatia matukio ya vurugu, uporaji wa mali na uvunjifu wa amani yaliyotokea tarehe Oktoba 29, mwaka huu katika majiji ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.

Pia katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara, Dodoma, Kilimanjaro na Iringa na kusababisha madhara kwa binadanu, kuharibu mali nyingi za umma na za watu binafsi na kulileta athari kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, mbali na athari kwa uhai na maisha ya watu, waliofanya uhalifu huo waliharibu na kuchoma moto mali za umma kama vile Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Maeneo mengine ni Mahakama, ATM za baadhi ya Benki, Vituo vya Polisi, Vituo vya Mabasi ya Mwendo kasi kutoka Kimara mwisho hadi Magomeni na kutoka Magomeni hadi Moroco, Ofisi za Serikali za Mitaa, kuchoma moto barabara za lami na za zege kwa kutumia matari na majengo kadhaa ya Chama cha Mapinduzi. Pia walichoma moto na kuharibu magari ya umma.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: