Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa ufafanuzi kukanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya jamii kuhusu vijana wawili wa mkoani humo waliodaiwa kutekwa na watu wasiojulikana.
"Taarifa sahihi ni kwamba kwa nyakati tofauti tuliwakamata na tunaendelea kuwahoji vijana hao ambao ni Edwin Richard Mboro (29) mkazi wa Sanawari Jijini Arusha na Victor Bonaventure Ndibalema (35) mkazi wa Kijenge kutokana na tuhuma za kupanga na kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria" imesema sehemu ya taarifa hiyo ya polisi.
Chanzo; Nipashe