Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chalamila Afika kwa Mjane Aliyetolewa Vitu Njee, Mikocheni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila leo September 24,2025 amefika Mikocheni kukutana na Alice Haule, Mjane wa marehemu Justice Rugaibula ambaye jana amevamiwa kwenye nyumba yake (nyumba namba 3) iliyoko Tembo Street, Mikocheni Bakharesa na Watu waliodai kuwa wametumwa na Mfanyabiashara Mohamed Yusufali ambaye kwa muda mrefu wamekuwa wakivutana kisheria Mahakamani kwa kesi tofauti za madai hata kabla ya mumewe kufariki baada ya Mohamed kudai nyumba hiyo ni yake na aliuziwa na Justice enzi za uhai wake mwaka 2011 na kwamba hata hati ya nyumba anayo Mfanyabiashara huyo.

Itakumbukwa Jana Mabaunsa walisukuma geti la nyumba hiyo ambayo kwa sasa imepangishwa kwa Raia wa Kichina na kuingia ndani na kuanza kuwashambulia Watu waliokuwa ndani sambamba na kuanza kutoa vitu nje kinyume na taratibu wakimtaka Mpangaji huyo wa Alice atoke kwakuwa nyumba imeshauzwa na baadaye video ya Alice ilisambaa mitandaoni akilalamika na kuomba asaidiwe kupata haki yake.

RC Chalamila amesema amemtaka pia Mohamed afike kwenye nyumba hii ili asikilize pande zote mbili ili haki itendeke na akiwa hapa Chalamila ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saada Mtambule na Maafisa kutoka Idara za ardhi pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: