Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watu watano kwa tuhuma za kumuua Hamza Malingumu (20) katika eneo la Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Polisi wamesema marehemu aliuawa baada ya kudhaniwa kuwa ni mwizi. Hata hivyo, mjomba wa marehemu, Ngwenje Mohamed, amesema kijana huyo alikuwa mgonjwa wa akili na alikuwa mgeni maeneo hayo akitokea Kilosa akidai alitoroka nyumbani majira ya saa tisa usiku bila mtu kujua alikokwenda.
"Kumbe walimwitia mwizi na watu kujitokeza na kumpiga hadi kupoteza fahamu,” amesema.
Amesema familia ilijaribu kumkimbiza hospitali, lakini alifariki dunia akiwa njiani. Polisi imesema uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea huku baadhi wakitiwa nguvuni kuhusiana na tukio hilo.
Chanzo; Nipashe