Baada ya Mgombea Urais wa chama kikuu cha upinzani National Unity Platform (NUP), Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) kudaiwa kutekwa na vyombo vya usalama na kupelekwa kusikojulikana usiku wa Januari 17, 2026, taarifa zimedai alifanikiwa kutoroka huku mke wake akiendelea kuwekwa chini ya ulinzi nyumbani kwake.
Kupitia Mtandao wa X (Twitter), mtoto wa Bobi Wine, Solomon Kampala amesema amepata taarifa kuwa wakati uvamizi ukiendelea baba yake alifanikiwa kutoroka lakini mama yake anaendelea kushikiliwa nyumbani kwao chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi huku hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia wala kutoka.
Haya yanatokea siku mbili baada ya Uganda kufanya Uchaguzi Mkuu, ambapo matokeo ya awali yakionyesha Yoweri Museveni anaongoza kwa Asilimia 76.25.
Chanzo; Jamii Forums