Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wamekutana katika makazi ya Mar-a-Lago, Florida, kwa mazungumzo nyeti yanayolenga dhamana za usalama wa Ukraine, huku juhudi za kutafuta suluhu ya vita dhidi ya Urusi zikiendelea.
Mkutano huo umefanyika siku chache baada ya Zelenskyy kusema kuwa alikuwa na mazungumzo mazuri na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff pamoja na Jared Kushner, mkwe wa Rais Trump.
Akizungumza na waandishi wa habari, Trump amesema anaamini kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko makini kuhusu amani.
“Nadhani yuko makini. Nadhani wote wawili wako tayari,” alisema Trump.
Trump pia alifichua kuwa alifanya mazungumzo mazuri na yenye tija kubwa na Putin siku ya Jumapili, kabla ya kukutana na Zelenskyy kauli inayoongeza uzito wa matarajio ya hatua mpya za kidiplomasia katika mgogoro wa Ukraine.
Chanzo; Cnn