Kwa kina mama wanaojifungua kabla ya wakati au wanaoshindwa kutoa maziwa ya kutosha, kutegemea maziwa ya kopo ambacho ni chakula kilichotengenezwa na kuuzwa kwa ajili ya kuwalisha watoto wachanga walio chini ya umri wa miezi 12 mara nyingi huambatana na aibu, na wasiwasi kuhusu ubora wa lishe.
Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema ni chini ya nusu ya watoto wachanga duniani wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee. Mpango wa uchangiaji wa maziwa ya mama ni suluhisho, lakini pia unakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kutosha hospitalini.\
Chanzo: Dw