Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watu Wenye Akili Zaidi Duniani Kwenye Picha ya Pamoja

Mwaka 1927, ulifanyika Mkutano wa Tano wa SolvayFifth Solvay huko Brussels, Ubelgiji na kuwakutanisha baadhi ya wanasayansi mashuhuri zaidi duniani.

Mkutano huu wa kihistoria ulikuwa na lengo la kujadili msingi wa mekaniki ya quantum. Ndipo ikapiwa picha hiyo maarufu ambayo hadi sasa imebaki kama kumbukumbu huku ikitambulika kwa jina la 'picha yenye akili zaidi duniani', ikionyesha kundi la watu wenye mchango mkubwa wa kisayansi.

Kati ya wanasayansi waliokuwepo, ni Marie Curie ambaye anaonekana mwanamke pekee katika kundi hili. Curie ni maarufu kutokana na utafiti wake juu ya radioactivity na ni mwanamke wa kwanza na mmoja tu kushinda Tuzo ya Nobel mara mbili. Moja katika Fizikia na nyingine katika Kemia.

Wanasayansi wengine katika picha hiyo ni Albert Einstein, Niels Bohr, Werner Heisenberg, Paul Dirac,Max Planck na wengineo.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: