Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Kamishna wa Tume ya Takwimu, masaa machache baada ya taasisi hiyo kutangaza kuwa uzalishaji ajira mpya wa Marekani umepungua.
“Nimepewa taarifa kwamba takwimu za ajira zinatengenezwa na mteule wa Biden, Dr Erika McEntrafer, Kamishna wa Takwimu za Ajira, ambaye alighushi namba za ajira kabla ya uchaguzi ili kuongeza uungwaji mkono kwa Kamala Harris ili ashinde, tunahitaji namba sahihi. Nimeagiza afutwe kazi mara moja. Nafasi yake itazibwa na mtu muadilifu na aliekidhi vigezo”, ameandika Trump kupitia mtandao wa Truth Social.