Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) imemtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu akipata asilimia 71.6 ya jumla ya kura halali zilizopigwa na kuendeleza utawala wake zaidi ya miongo minne.
Mpinzani wake Mkuu, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amepata asilimia 24.72 ya kura zote zilizopigwa.
Bobi Wine ambaye amedaiwa kukimbia nyumbani kwake baada ya polisi kuvamia jana Ijumaa, amekataa matokeo hayo ya uchaguzi akidai kuwa ni ya uongo.
Chanzo; Mwananchi