Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Al-Sharaa Atua Marekani Baada Kondolewa Kwenye Orodha ya Magaidi

Rais wa Syria, Ahmed al-Sharaa amewasili Marekani jana usiku kwa ziara rasmi ya kihistoria, kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Syria, siku moja baada ya Washington kuliondoa jina lake kwenye orodha yake ya magaidi.

Saa chache kabla ya kuwasili kwake katika mji mkuu wa Marekani taarifa ziliibuka kuwa vyombo vya usalama vya Syria vimewakamata makumi ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi linalojiita Islamic State.

Al-Sharaa anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu, ikiwa ni ziara ya kwanza ya aina hiyo kufanywa na rais wa Syria tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mwaka 1946.

Juhudi za pamoja za kukabiliana na mabaki ya kundi hilo nchini Syria zinatarajiwa kuwa ajenda kuu wakati wa mazungumzo ya Sharaa na Trump.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: