Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

UE Kutoa Mafunzo kwa Polisi 3,000 Gaza

Umoja wa Ulaya (EU) unafikiria kutoa mafunzo kwa maofisa wa polisi takribani 3,000 katika Ukanda wa Gaza, sawa na kile ambacho tayari umefanya katika Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, hayo yamebainishwa leo na ofisa mmoja wa Ulaya aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, akisema; "kutakuwa na haja ya kuimarisha Gaza kwa kikosi kikubwa cha polisi.”

Siku chache zilizopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa azimio linalounga mkono mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump, ambao ulisababisha utekelezaji wa kusitisha mapigano, Oktoba 10, mwaka huu kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Israel na Hamas, kundi la wanamgambo wa Palestina, walifikia makubaliano mnamo Oktoba kuhusu awamu ya kwanza ya mpango wa utekelezaji, lakini utekelezaji wa vipengele vingine vya makubaliano haya bado haujabainika.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: