Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

DRC Yakanusha Kuuza Madini kwa Marekani

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekanusha madai kwamba imeuza utajiri wake mkubwa wa madini kwa Marekani kupitia makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana yanayoruhusu Washington kufikia hifadhi yake kubwa ya madini.
Matamshi hayo yametolewa na Waziri wa madini wa nchi hiyo Louis Watum katika mkutano wa African Mining Indaba uliofanyika mjini Cape Town siku ya Jumatano. Watum amenukuliwa akisema kuwa “DRC haijauza kitu chochote kabisa” kupitia makubaliano hayo na Washington.

Makubaliano hayo, yaliyosainiwa mwezi Desemba sambamba na mkataba wa amani unaolenga kukomesha mgogoro wa muda mrefu mashariki mwa DRC, yanafungua njia kwa Marekani kuyafikia madini kama shaba, cobalt, coltan na lithium, wakati Washington inapojaribu kupunguza kutegemea mtandao wa uzalishaji wa madini muhimu unaoongozwa na Beijing.

 

 

Chanzo; Dw

Kuhusiana na mada hii: