Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Zao la Bangi la Ruhusiwa Brazil

Wakala wa Taifa wa Udhibiti wa Afya wa Brazil (Anvisa) imeruhusu rasmi, Jumatano Januari 28, kilimo cha mmea wa Cannabis Sativa (bangi) nchini humo kwa matumizi ya tiba na utafiti wa kisayansi.

Uamuzi huo umetokana na maelekezo ya Mahakama ya Juu ya Haki (STJ), ambayo Novemba, 2024 ilithibitisha uhalali wa uzalishaji wa bangi kwa madhumuni ya tiba na/au dawa pekee, kama sehemu ya kulinda haki ya afya.

Kwa matumizi ya tiba, wakurugenzi wa Anvisa wameidhinisha kwa kauli moja kilimo cha katani ya viwandani (industrial hemp) aina maalumu ya Cannabis sativa yenye kiwango cha tetrahydrokannabinoli (THC) kisichozidi asilimia 0.3. THC ndiyo kiungo kikuu kinachosababisha athari za kisaikolojia.

Aina hii ya bangi haisababishi kulewa, lakini ina kiwango kikubwa cha cannabidiol (CBD), ambayo inathaminiwa kwa uwezo wake wa tiba katika kusaidia wagonjwa wenye wasiwasi (anxiety), maumivu sugu, kifafa, matatizo ya usingizi, pamoja na magonjwa mengine ya mfumo wa neva.

Kwa mujibu wa kanuni mpya, uzalishaji utakuwa na mipaka kulingana na mahitaji ya dawa. Kampuni zitawajibika kutoa taarifa kamili kuhusu kiasi kinachozalishwa, sababu za uzalishaji huo, pamoja na ukubwa wa ardhi (hekta) itakayotumika kwa kilimo.

Aidha, kilimo hicho hakijaruhusiwa kwa umma kwa jumla; kinaruhusiwa kwa kampuni na mashirika maalumu pekee. Hatua hii haijumuishi matumizi ya burudani ya bangi, bali inalenga tiba na utafiti wa kisayansi pekee.

 

 

Chanzo; Global Publishers

 

 

 

Kuhusiana na mada hii: