Wapiga kura nchini Uganda walijitokeza kupiga kura Januari 15, 2026 kwa uchaguzi wa rais na wabunge, lakini mchakato huo ulikumbwa na changamoto baada ya mashine za uthibitishaji wa alama za vidole (biometriki) kushindwa kufanya kazi katika vituo vingi vya kupigia kura.
Kutokana na hitilafu hizo, maafisa wa uchaguzi walilazimika kurejea matumizi ya daftari la maandishi (manual registers), hali iliyosababisha ucheleweshaji na misururu mirefu ya wapiga kura katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Licha ya changamoto hizo za kiufundi, wapiga kura wengi waliendelea kushiriki zoezi hilo, wakionyesha dhamira yao ya kutumia haki yao ya kidemokrasia chini ya mazingira magumu.
Chanzo; Cnn