Wanajeshi wanne wa Urusi wameeleza kwa kina hali ya ukatili na mateso waliyoishuhudia katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine.
Wawili kati yao walithibitishia BBC kuwa waliona wanajeshi wakipigwa risasi na kuuawa papo hapo kwa sababu ya kukataa kutekeleza amri za kijeshi.
Mmoja wao alisema kwamba alimwona mwanajeshi akiuawa kwa amri ya kamanda wake, kamanda ambaye baadaye alitunukiwa cheo cha Shujaa wa Urusi mwaka 2024.
Mwanajeshi mwingine kutoka kikosi tofauti alieleza kuwa alimwona kamanda wake akiwapiga risasi watu wanne kwa mikono yake mwenyewe.
"Niliwajua, nakumbuka mmoja wao akipaza sauti: 'Usinipige risasi, nitafanya chochote utakachosema,” alisema.
Mtu mwingine alisimulia kuwa aliona miili ya wanajeshi wenzake ishirini ikiwa imetupwa kwenye shimo baada ya "kuondolewa", neno la msimu wa kijeshi wa Urusi linalomaanisha kumuua mwanajeshi mwenzako.
Chanzo; Nipashe