Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Iran Yashambulia Kambi za Marekani

Baada ya mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran asubuhi ya leo Jumamosi, Tehran imejibu kipigo kwa kulenga washirika wa Marekani.

Milipuko na ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika katika mji mkuu wa Qatar, Doha.

Wizara ya ulinzi ya Qatar imesema imefanikiwa kukabiliana na mashambulizi kadhaa yaliyolenga eneo la nchi hiyo.

Afisa mmoja wa Qatar ameliambia shirika la habari la AFP kwamba betri ya Patriot iliyotengenezwa Marekani ilinasa kombora la Iran.

Qatar ni mwenyeji wa kambi ya kijeshi ya Al Udeid, kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani katika eneo hilo la mashariki ya kati.

Vile vile, Iran haikukomea hapo, ililipua kambi za jeshi la Marekani nchini Bahrain, UAE na Kuwait na Kambi hizo ni kama vile kambi ya Al Salem, Al Dhafra, Al Udeid na pia Makao ya Kikosi cha 5 cha Jeshi la Wanamaji la Marekani yashambuliwa nchini Bahrain.

Mashambulizi yanaendelea na hayajulikani muafaka utaafikiwa lini.

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: