Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Maduro Mahakamani, Trump Atishia Kuongeza Mashambulizi

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Shirikisho ya Marekani mjini New York leo Jumatatu Januari 5, 2026, kufuatia kukamatwa kwake mwishoni mwa wiki katika oparesheni ya kijeshi iliyoendeshwa na majeshi ya Marekani mjini Caracas, Venezuela.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Marekani itachukua hatua nyingine za kijeshi endapo Venezuela haitashirikiana na juhudi za Marekani kufungua sekta ya mafuta na kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumapili, Trump amesema anaweza kuamuru shambulio jingine ikiwa masharti hayo hayatatimizwa.

Kauli ya Trump inakuja wakati kukiwa na sintofahamu kubwa kuhusu mustakabali wa Venezuela, baada ya kukamatwa kwa Maduro Jumamosi katika uvamizi wa kijeshi uliosababisha wasiwasi wa kimataifa.

Maduro na mkewe, Cilia Flores, wanakabiliwa na mashtaka nchini Marekani ya kula njama ya ugaidi wa mihadarati, kula njama ya kuingiza dawa za kulevya (kokeini) nchini humo pamoja na makosa yanayohusiana na silaha.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: