Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulizuka katika Ukumbi ambao ndani yake mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi nchini Brazil ulikuwa ukiendelea jana Alhamisi Novemba 20 na kuwalazimu wajumbe kukimbilia sehemu salama..
Wakati Waziri wa Utalii wa Brazil Celso Sabino akitangaza kudhibitiwa kwa moto huo, ulioanza saa nane mchana huku ikiripotiwa kuwa hakuna aliyeumia, maswali mengi yameibuka kuhusu athari kwenye mkutano huo wa kilele, ambao umefikia awamu ya kuamua kama utafanikiwa au kushindwa.
Chanzo; Eatv