Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kushirikiana na Marekani kuhusu mpango wa kumaliza vita na Urusi. Amesema baada ya mazungumzo na Afisa anayesimamia masuala ya Jeshi la Marekani Daniel Driscoll.
Aliyasema haya baada ya mazungumzo na Waziri anayesimamia masuala ya Jeshi la Marekani Daniel Driscoll, na anatarajia kujadili mapendekezo hayo na Rais wa Marekani Donald Trump katika siku chache zijazo.
Maelezo ya mpango huo hayajawekwa wazi, lakini ripoti zinadokeza kuwa unajumuisha makubaliano mapana kwa Urusi, ukiitaka Ukraine kupunguza nusu ya ukubwa wa jeshi lake na kuachilia majimbo ya mashariki yanayokaliwa na Urusi ikiwa ni pamoja na Donetsk na Luhansk.
Ikulu ya White House inasema mpango huo ni “mzuri kwa pande zote mbili” na inathibitisha uungwaji mkono wa Trump, licha ya wasiwasi kwamba unaakisi matakwa ya Urusi. Ukraine inasisitiza kwamba makubaliano yoyote lazima yawe uhakikisho wa kweli wa usalama kutoka nchi za Magharibi ili kuzuia mashambulizi ya siku zijazo.
Maafisa wakuu wa Umoja wa Ulaya, Poland na Ujerumani wametoa kauli za mashaka kuhusu ripoti ya mpango huo wakisema ili mpango wowote wa amani ya Ukraine ufanye kazi, unahitaji ushirikishwaji wa raia wa Ukraine na Ulaya.
Chanzo; Bongo 5