Waziri Mkuu mpya wa Japan Sanae Takaichi wiki iliyopita aliwaamuru wafanyakazi wake kuripoti ofisini saa tisa usiku.
Katika taifa ambalo watu hufariki mara kwa mara kutokana na kufanya kazi kupita kiasi, hali inayojulikana kama karoshi Takaichi amekiri kwamba hulala kwa takriban saa mbili pekee au ikizidi sana, hulala kwa saa nne, akisisitiza umuhimu wa nidhamu ya kazi.
Wakati akiwaamuru wafanyikazi waripoti kazini saa tisa usiku, Waziri Mkuu huyo wa Japan aliripotiwa kuhitaji kupitia nyaraka muhimu baada ya mashine ya fax nyumbani kwake kushindwa kufanya kazi.
Takaichi anajilinganisha na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher ambaye alijulikana kwa kuwaamsha wasaidizi wake usiku wa manane kwa mtazamo huo, Takaichi anapenda kujiona kama Iron Lady wa Japan.
Bosi Awaamuru Wafanyakazi Waripoti Kazini Saa Tisa Usiku
- Chanzo:
- Dw