Tathmini mpya iliyotolewa leo Alhamisi inaonesha uhuru wa kutumia intaneti umeporomoka nchini Marekani na Ujerumani katika wakati nchi kadhaa za magharibi zimetumbukia kwenye mkondo sawa na tawala za kimabavu kwa kuweka vizuizi mitandaoni.
Kwenye taarifa yake ya hadi katikati mwa mwaka huu, taasisi ya Freedom House yenye makao yake nchini Marekani imesema uhuru wa kutumia mtandao umeanguka kwa mwaka wa 15 mfululizo huku kiwango cha ukandamizaji na udhibiti kimeongezeka katika nchi zilizozingatiwa hapo kabla kuwa na uhuru.
Marekani na Ujerumani ni miongoni mwa mataifa yaliyozidisha udhibiti wa matumizi ya intaneti kwa kuweka kanuni kali za kutoa maoni mtandaoni.
Mzozo wa Gaza, kushamiri kwa siasa kali za kizalendo na kurejea madarakani kwa Donald Trump ni miongoni mwa mambo yaliyoongeza udhibiti wa maoni mitandaoni.
Kenya nayo imetajwa hasa kutokana na kuufunga mtandao wa intaneti wakati wa maandamano ya umma.
Chanzo; Dw