Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Rais wa Zamani Brazil Jela Miaka 27, hatia Njama Kupindua Matokeo ya Uchaguzi

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 Gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kupanga njama za kupindua matokeo ya uchaguzi wa Urais wa mwaka 2022 Nchini humo na kujaribu kubaki madarakani kwa nguvu.

Mahakama ya Juu ya Brazil imemkuta Bolsonaro na hatia kwa makosa matano ikiwemo kupanga mapinduzi ya Serikali, kushiriki katika Genge la uhalifu lenye silaha, kufanya jaribio la kuondoa utawala wa kidemokrasia kwa nguvu, kufanya vurugu dhidi ya Taasisi za Serikali na kuharibu mali za Umma wakati wa uvamizi wa majengo ya Serikali na Wafuasi wake Januari 8, 2023.

Jopo la Majaji watano wa Mahakama hiyo lilipiga kura ambapo Majaji wanne waliunga mkono kumtia hatiani Bolsonaro huku Waendesha mashtaka wakisema kuwa sehemu ya mpango huo ilikuwa njama ya kutumia mabomu, silaha za kivita au sumu kumuua Rais Luiz Inácio Lula da Silva, Makamu wa Rais Geraldo Alckmin na Jaji wa Mahakama ya Juu Alexandre de Moraes, ambaye ndiye alisimamia kesi hiyo.

Polisi wa Shirikisho walieleza kuwa Bolsonaro alikuwa na taarifa kamili kuhusu mpango wa kupindua matokeo ya uchaguzi, kushinikiza Jeshi kuingilia kati na hata kuandaa Ofisi mbadala ya “usimamizi wa mgogoro” ili kuendesha Serikali ambapo inadaiwa mpango huo ulianza mwaka 2021 kwa juhudi za kudhoofisha imani ya umma katika mfumo wa uchaguzi na baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2022, Washitakiwa walihamasisha Wafuasi kuvamia na kuharibu mihimili mitatu ya Serikali mjini Brasília.

Hata hivyo Bolsonaro na wenzake walikanusha mashitaka hayo katika kesi hii na kudai kuwa hawakuhusika na njama yoyote ya kupindua Serikali.

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: