Huu ndio wakati maafisa wa uhamiaji nchini Marekani walipompiga risasi na kumuua mwanamke mmoja mzungu kwenye mji wa Minneapolis. Maafisa hao walikuwa kwenye msako --ambao ni sehemu ya kampeni pana ya Rais Donald Trump ya kudhibiti wahamiaji wasio na vibali tangu aliporejea madarakani Januari mwaka jana.
Kwenye mkanda wa video ulionaswa na shuhuda wa tukio hilo, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 alionekana akitaka kuondoka na gari yake kwa nguvu kabla ya afisa uhamiaji mwenye bunduki kufyetua risasi iliyomuua papo hapo.
Rais Trump ametetea tukio hilo akisema, afisa huyo alitimiza wajibu wake "wa kujilinda."
Hata hivyo, maandamano makubwa yamezuka kwenye mji huo kulaani kisa hicho.
Chanzo; Dw