Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kimbunga Kalmaegi Chatinga Vietnam

Baada ya kupita Ufilipino, kimbunga Kalmaegi kimeingia Vietnam usiku wa kuamkia Ijumaa na kuua takribani watu watano, wakiwemo watatu katika mkoa wa Đắk Lắk na wawili wa Gia Lai. Zaidi ya nyumba 2,600 zimeharibiwa na takribani watu milioni 1.3 wamepoteza umeme. Serikali ya Vietnam imeonya kuhusu hatari ya mafuriko na mmomonyoko wa ardhi, hasa katika maeneo ya milimani na mashambani.

Kalmaegi, inayojulikana pia kama Tino nchini Ufilipino, imeendelea kusababisha maafa makubwa katika nchi za Asia ya Kusini Mashariki, ambapo idadi ya vifo nchini Ufilipino imefikia takriban watu 188, huku wengine 135 wakiwa hawajulikani walipo, kwa mujibu wa mamlaka ya ulinzi wa raia nchini humo.

Mikoa ya Cebu, Visayas na Mindanao ndiyo imeathirika zaidi, nyumba na miundombinu mingi ikiharibiwa vibaya. Serikali ya Ufilipino imetangaza hali ya dharura ya kitaifa ili kurahisisha shughuli za uokoaji na utoaji wa misaada kwa maelfu ya watu waliopoteza makazi. Wataalamu wa hali ya hewa wanasema Kalmaegi ni moja ya tufani zenye nguvu zaidi kuwahi kukumba taifa hilo mwaka huu, ikiambatana na mvua kubwa na upepo uliofikia zaidi ya kilomita 180 kwa saa.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: