Afisa mmoja mkuu wa jeshi nchini Nigeria Waidi Shaibu, amewaamuru wanajeshi wake kupigana "mchana na usiku" ili kuwaokoa wasichana 25 wa shule waliotekwa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Shaibu ambaye hivi karibuni alipandishwa cheo kuwa mkuu wa jeshi, ameaviambia vikosi vilivyopelekwa jana katika jimbo la Kebbi kwamba lazima viendeleze juhudi za kuwatafuta wasichana hao.
Ingawa polisi waliharakisha kufika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana katika mji wa Maga, genge hilo lilifanikiwa kuwateka nyara wanafunzi hao baada ya kumuua naibu mkuu wa shule hiyo.
Uvamizi huo wa jana asubuhi, ni wa hivi punde zaidi katika msururu wa utekaji nyara wa watoto wa shule kaskazini mwa Nigeria, zaidi ya muongo mmoja baada ya Boko Haram kuwateka nyara wasichana 276 kaskazini mashariki , tukio lililozua taharuki ya kimataifa.
Chanzo; Dw