Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Akiri Marekani Kutaka Mafuta ya Venezuela

Akiwa katika uwanja wa ndege wa jeshi wa Joint Base Andrews Jumatano ya Desemba 17, 2025 Rais wa Marekani Donald Trump alikiri kwamba Marekani inataka “mafuta yao” waliyonyang’anywa baada ya serikali ya Hugo Chavez, mtangulizi wa Nicolás Maduro, kutaifisha makampuni ya uchimbaji mafuta ya Kimarekani.

“Tunataka yarudishwe. Walichukua haki zetu za uchimbaji mafuta - tulikuwa na mafuta mengi huko. Kama unavyojua waliyafukuza makampuni yetu, na tunataka yarudishwe.” Alisema Trump.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2007, aliyekuwa Rais wa Venezuela wakati huo Hugo Chávez alimalizia hatua kubwa aliyoianza miaka mingi nyuma ya kutaifisha makampuni ya mafuta ya Marekani yaliyokuwa yakifanya kazi katika ukanda wa Orinoco. Uamuzi huu ulikuwa sehemu ya sera yake ya “Mapinduzi ya Kijamaa ya Karne ya 21,” iliyolenga kurejesha udhibiti wa rasilimali muhimu mikononi mwa serikali ya Venezuela.

Chávez aliamini kuwa kwa miongo mingi, makampuni ya kigeni yalikuwa yakinufaika zaidi na utajiri wa mafuta wa nchi hiyo huku wananchi wa kawaida wakibaki katika umaskini.

Serikali yake ilibadilisha mikataba ya zamani na kuhitaji kwamba miradi yote mikubwa ya mafuta iwe chini ya umiliki wa wengi wa kampuni ya taifa, PDVSA. Makampuni ya Marekani kama ExxonMobil na ConocoPhillips yalitakiwa kukubali masharti mapya au kuondoka nchini. Baadhi ya makampuni yaliondoka baada ya kushindwa kufikia makubaliano, na baadaye yakafungua kesi za madai ya fidia katika mahakama za kimataifa.

Chávez alitetea hatua hiyo akisema ilikuwa ya kisheria na ya haki, kwa kuwa rasilimali za asili zinapaswa kuwanufaisha wananchi wote. Mapato ya mafuta yalielekezwa kwenye elimu, afya, na miradi ya kijamii. Hata hivyo, kutaifisha huko kulizidisha mvutano kati ya Venezuela na Marekani, na kuchangia kupungua kwa uwekezaji wa kigeni

 

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: