Umati wa watu umekusanyika Minneapolis, Marekani kupinga uwepo wa maafisa wa uhamiaji wa shirikisho katika jimbo hilo, baada ya kupigwa risasi na kuuawa Alex Pretti mwenye umri wa miaka 37.
Gavana wa Minnesota Tim Walz ametoa wito kwa Rais wa Marekani, Donald Trump kuwaondoa maafisa hao wa shirikisho katika jimbo lake, akisema: "Huu ni wakati wa mabadiliko."
Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Walz na Meya wa Minneapolis Jacob Frey wanapaswa kuwasalimisha "wahamiaji wote haramu wahalifu" waliofungwa katika magereza ya Serikali kwa ajili ya kuwafukuza nchini.
Maafisa wa jimbo na shirikisho wametoa maelezo yanayokinzana kuhusu tukio la kifo cha Pretti siku ya Jumamosi.
Alipoulizwa kuhusu video zilizoibuka zikionyesha tukio hilo la mauaji, Kamanda wa Doria ya Mpakani Greg Bovino anasema kuna haja ya kuwepo kwa uchunguzi ili kubaini ukweli.
Chanzo; Itv