Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uchaguzi Uganda Serikali Yazima Matangazo Mubashara, Upinzani Walalamika

Serikali ya Uganda imeweka masharti mapya yanayozuia vyombo vya habari kurusha matangazo ya moja kwa moja ya ghasia, maandamano yasiyoidhinishwa na matukio ya vurugu, siku chache kabla ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Januari 15, 2026.

Kupitia agizo lililotolewa Januari 5 na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, serikali imesema hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa umma na kuzuia kuchochea taharuki wakati wa kipindi nyeti cha kisiasa.

Mamlaka ya Mawasiliano Uganda (UCC) imeonya kuwa itachukua hatua kali dhidi ya vyombo vya habari vitakavyokiuka agizo hilo, ikisisitiza kuwa matangazo ya mubashara yanaweza kuchochea vurugu au kusambaza chuki.

UCC pia imewakumbusha waandishi wa habari kuwa kutangaza matokeo ya uchaguzi ni jukumu la Tume ya Uchaguzi pekee, na kwamba kuchapisha au kurusha takwimu zisizo rasmi ni kosa la kisheria.

Hata hivyo, upinzani na mashirika ya haki za binadamu wamekosoa vikali hatua hiyo, wakisema ni njama ya kuzima uhuru wa vyombo vya habari na kuficha vitendo vya ukandamizaji.

Wakosoaji wanasema serikali imekuwa ikitaja hata maandamano ya amani kama “ghasia”, hali inayozua hofu kuwa marufuku hiyo itatumika kuzuia taarifa halali za kisiasa.

Kiongozi wa upinzani Bobi Wine ameituhumu serikali kwa kuendesha kampeni ya vitisho, kukamata kiholela na kutumia nguvu dhidi ya wafuasi wake madai ambayo serikali imeyakanusha.

 

 

 

Chanzo; Cnn

Kuhusiana na mada hii: