Waasi wa AFC/M23 hii leo Alhamisi (08.01.2026) wamefanya mazishi ya miili ya watu 22 waliouawa katika mashambulizi yaliyofanywa na droni za serikali ya Kinshasa mnamo kipindi cha miezi miwili iliopita.
Waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda, wanaituhumu serikali ya Rais Felix Tshisekedi kuhusika na mashambulizi ya droni katika maeneo wanakoishi raia.
Shambulizi la hivi karibuni ni lile la tarehe 2 Januari, katika mji wa Masisi, jimboni Kivu Kaskazini, unaokaliwa na waasi wa M23, ambako watu 6 waliuawa na wengine zaidi ya ishirini kujeruhiwa.
Chanzo; Dw