Mke wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na kiongozi wa upinzani kwa muda mrefu, hayati Raila Odinga, Ida Odinga, ameweka wazi kuwa utajiri wake binafsi unakadiriwa kuwa shilingi milioni 500 sawa na dola za Marekani milioni 3.9.
Ameyasema hayo alipofika mbele ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mahusiano ya Kigeni ikiwa ni sehemu ya mchakato wa uthibitisho wa uteuzi wake kama Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP).
Amesisitiza kuwa utajiri alioutaja ni wake binafsi na kwamba haujumuishi mali za familia pana ya Odinga.
Bi. Ida amebainisha kuwa mali za ukoo wa Oginga Odinga ni pana na zimepatikana kwa miongo kadhaa, lakini alichagua kuwasilisha tu mali zinazomhusu yeye binafsi.
Chanzo; Dw