Mamlaka ya mawasiliano ya Uganda yameagiza kusitishwa kwa huduma za intaneti ya umma kote nchini kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika wiki hii Januari 15.
Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) inasema hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa taifa na uadilifu wa zoezi la upigaji kura.
Hata hivyo, wakosoaji wanasema uamuzi huo unadhoofisha uwazi na unakinzana na ahadi za awali zilizotolewa na serikali.
Chanzo; Bbc