Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Charlie Apigwa Risasi Aliacha Shule Aitumikie Siasa Muda Wote

Charlie Kirk alikuwa mwanaharakati kijana wa kisiasa wa Marekani alizaliwa tarehe 14 Oktoba 1993 huko Arlington Heights, Chicago, Illinois, Marekani na kulia maeneo ya jirani kama Prospect Heights. Mama yake, alikuwa mshauri wa afya ya akili, na baba yake mzee, Robert, alikuwa mbunifu. 

Charlie alisoma shule Wheeling High School, ambapo alianza kushiriki katika siasa, akisaidia kampeni za seneta wa chama cha Republican, Mark Kirk, licha ya kufanana ubini hawakuwa na undugu wowote. Charlie hakumaliza Chuo kikuu cha Harper College kwa sababu aliamua kuitumikia siasa kwa muda wote, akiongozwa na harakati za Tea Party.

Jamii ya wanamarekani inamtambua kama kiongozi wa vijana na rafiki wa karibu wa Rais Donald Trump. Alianzisha TPUSA mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 18. Shirika ambalo lilifundisha kuhusu uhuru wa uchumi, haki ya kumiliki silaha, na maadili ya Kikristo, huku likipinga mawazo na sera za chama cha Demokrasia. 

Pia Charlie alikuwa mtangazaji wa kipindi cha redio "The Charlie Kirk Show" na aliandika vitabu kama "Time for a Turning Point" mwaka 2016. Alipigania masuala kama chanjo za COVID-19, na aliamini maono ya Kikristo kama creationism, pia moja ya mpinzani mkubwa wa mapenzi ya jinsia moja. Alikuwa na ushawishi mkubwa katika kampeni za Trump za 2016, 2020, na 2024, na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Septemba 2025, Charlie Kirk aliuawa kwa kupigwa risasi wakati akizungumza kwenye tukio la TPUSA lililoitwa "American Comeback Tour" katika Chuo Kikuu cha Utah Valley, Orem, Utah. Tukio hilo lilifanyika dakika 20 tu baada ya kuanza, mbele ya hadhira ya watu karibu 3,000. 

Mkewe na watoto wawili walikuwepo wakati wa tukio. Mpaka sasa Polisi na FBI wamepata bunduki iliyotumika na wameona picha za mshukiwa, ambaye ni mwanafunzi wa chuo mwenye uzoefu wa silaha. Ripoti za hivi karibuni zinasema mshukiwa amekamatwa baada ya kujisalimisha kupitia baba yake na mchungaji wake. Uchunguzi bado unaendelea, na viongozi kama Trump na Netanyahu wametoa salamu za pole.

Zaidi, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kupepea bendera nusu mlingoti muda mchache mara baada ya tukio kutokea.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: