Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

SADC Bado Kinara Duniani Mapambano ya HIV

 Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimisha mafanikio yake katika kupambana na UKIMWI, ikiwa ni mojawapo ya maeneo yanayoongoza duniani katika utoaji wa huduma za kuzuia maambukizi mapya na kupunguza vifo vinavyohusiana na UKIMWI.

Uongozi wa kikanda, kupitia Mkurugenzi wa UNFPA kwa Afrika Mashariki na Kusini, Lydia Zigomo, amesema SADC imepiga hatua kubwa kwa kupunguza maambukizi mapya na vifo, kutokana na mikakati thabiti ya uzuiaji na matibabu. Aidha, juhudi za kuweka haki za uzazi na upangaji uzazi katikati ya sera za maendeleo zinaonekana kutekelezeka vizuri.

Hata hivyo, Zigomo ametoa tahadhari kwamba mafanikio haya ni nyeti na yanaweza kuporomoka ikiwa mikakati haitaimarishwa zaidi, hasa kwa vijana, wanawake na wasichana ambao bado wanabeba mzigo mkubwa wa magonjwa haya.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: