Marekani imetangaza hii leo kuzipatia nchi mbili za Afrika dawa mpya ya kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi inayofahamika kama Lenacapavir.
Zambia na Eswatini zitaanza kutoa chanjo hiyo wiki hii ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Rais Donald Trump kupunguza kwa kiasi kikubwa misaada ya kigeni.
Lenacapavir ni tiba mpya ya sindano dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi-VVU ambayo inahitaji kutumiwa mara mbili tu kwa mwaka.
Kulingana na wataalamu, hii ni hatua kubwa mno ikilinganishwa na matibabu ya sasa ya kutumia kidonge kimoja kila siku.
Chanzo; Dw