Kamanda Mkuu wa M23, Sultani Makenga, amenusurika kuuawa baada ya kuondoka eneo la Rubaya dakika chache kabla ya shambulio la droni lililomuua msemaji wa kundi hilo, Willy Ngoma.
Shambulio hilo limesababisha vifo vya watu wengine tisa karibu na kitovu cha uzalishaji wa coltan kinachodhibitiwa na M23.
Wachambuzi wanasema kuuawa kwa Ngoma kunaweza kuongeza mvutano katika juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Qatar, ambazo tayari zimekuwa zikikumbana na vizingiti.
Wakati huohuo, mapigano yanaendelea Masisi kati ya M23, jeshi la Congo na makundi ya wazalendo, huku M23 ikidai serikali “imeanzisha vita kamili” katika Kivu Kaskazini na Kusini.
Chanzo; Dw