Minneapolis, Marekani Maandamano yamegeuka kuwa mapambano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa Ulinzi wa Mipaka wa Marekani (US Border Patrol) nje ya kituo cha ICE mjini Minneapolis, huku polisi wakitumia dawa ya pilipili na risasi za plastiki kuwatawanya waandamanaji.
Maandamano hayo yalizuka kufuatia tukio la kushtua la kuuawa kwa mwanamke mmoja kwa kupigwa risasi na afisa wa ICE wakati wa oparesheni ya utekelezaji wa sheria jimboni Minnesota, Jumatano.
Mashuhuda wanasema hasira za wananchi zililipuka nje ya jengo la ICE, wakilaani kile walichokiita matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia, huku mamlaka zikidai hatua zilizochukuliwa zilikuwa kwa ajili ya kujilinda na kurejesha utulivu.
Tukio hilo limeongeza mvutano mkubwa kuhusu oparesheni za uhamiaji na matumizi ya nguvu na vyombo vya usalama nchini Marekani.
Chanzo; Cnn