Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waliofunga Ndoa Ya Bilioni 2 Kuchunguzwa Kodi

Mamlaka ya Mapato ya Shirikisho la Pakistan (FBR) imeanza kufanya uchunguzi wa harusi ya kifahari ya Wageni 400 iliyogharimu karibu rupia milioni 248 ambazo ni zaidi ya Tsh. shilingi Bilioni mbili.

Kwa mujibu wa NDTV, sherehe hiyo ya siku nne ilihusisha mapambo ya kuvutia, mavazi ya Wabunifu wakubwa wa Asia Kusini, seti za dhahabu na almasi, chakula cha kifahari kwa Wageni 400 na onesho la droni angani, DJs, Wanamuziki wa Qawwali na Washauri wa Kimataifa wa kupanga matukio.

FBR wamesema gharama kubwa za harusi hiyo hazilingani na taarifa za mapato zilizotolewa na familia zilizohusika ambapo kitengo kipya cha Lifestyle Monitoring Cell kimepewa jukumu la kufuatilia mitandao ya kijamii kama Instagram, TikTok na YouTube ili kubaini matumizi ya kifahari yanayozidi uwezo wa kipato kilichotangazwa.

Kwa mujibu wa Maafisa, kitengo hicho kinaunda hifadhidata ya kidijitali ikijumuisha vielelezo vya picha za skrini, video na nyaraka ili kusaidia kesi za ukwepaji kodi na uchunguzi wa utakatishaji fedha ambapo harusi hii imekuwa moja ya kesi za kwanza kuchunguzwa.

Pakistan kwa muda mrefu imekuwa na kiwango cha chini cha ukusanyaji kodi Barani Asia huku chini ya asilimia 2 ya Wananchi wakilipa kodi ya mapato ambapo uchunguzi wa harusi hii unakuja katika kipindi ambacho Nchi hiyo inakabiliwa na shinikizo la kutimiza malengo ya mapato yaliyoainishwa kwenye bajeti inayoungwa mkono na Shirika la Fedha Duniani IMF.

 

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: