Wabunge wa Marekani jana walianza kupitia nyaraka zisizofichwa za Jeffrey Epstein, na kuonyesha wasiwasi baada ya kubaini kuwa baadhi ya majina yameeondolewa katika toleo lililotolewa kwa umma.
Sheria mpya ya uwazi wa nyaraka za Epstein EFTA iliyopitishwa kwa wingi na Bunge, ilitaka wizara ya Sheria kutoa kila hati waliyonayo kuhusu Epstein—bila kuondoa chochote kinachoweza kumlinda mtu kutokana na aibu, madhara ya sifa, au sababu za kisiasa.
Hata hivyo, sheria hiyo iliruhusu kufichwa kwa majina ya zaidi ya waathiriwa 1,000 wa Epstein ili kulinda utambulisho wao.
Chanzo; Dw