Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watu 200 Wafariki Dunia Mgodini DRC

Watu wasiopungua 200 wanahofiwa kupoteza maisha wiki hii baada ya maporomoko ya ardhi kuvuruga migodi kadhaa ya uchimbaji wa madini ya coltan mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Akizungumza na Associated Press, Lumumba Kambere Muyisa, msemaji wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini linalodhibitiwa na waasi wa M23, amesema tukio hilo lilitokea Jumatano katika migodi ya Rubaya, wilayani Masisi—eneo linalodhibitiwa na waasi hao.

Amesema maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa, huku watu kadhaa wakijeruhiwa na kukimbizwa katika vituo vitatu vya afya vilivyopo Rubaya. Ameongeza kuwa magari ya wagonjwa yanatarajiwa kuwahamisha majeruhi hao Jumamosi hii kuelekea Goma, jiji lililo umbali wa takribani kilomita 50, kwa ajili ya matibabu zaidi.

Ikumbukwe kuwa Mei 2024, kundi la M23 liliteka eneo la Rubaya na kudhibiti migodi yake. Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, tangu lilipotwaa Rubaya, kundi hilo limekuwa likitoza kodi kwenye biashara na usafirishaji wa coltan, na kujipatia angalau dola 800,000 za Marekani kwa mwezi.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: