Takribani watu 25 wamepoteza maisha kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Jumatatu jioni katika jimbo la Minas Gerais, kusini-mashariki mwa Brazil, na kusababisha mafuriko makubwa pamoja na maporomoko ya ardhi.
Kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo, watu 18 walifariki katika mji wa Juiz de Fora, huku wengine saba wakiripotiwa kupoteza maisha katika mji wa Ubá.
Idadi ya vifo inahofiwa kuongezeka, baada ya watu kadhaa kuripotiwa kupotea kufuatia kuporomoka kwa nyumba na majengo wakati wa mvua hiyo kubwa iliyonyesha usiku.
Mamlaka zimeendelea kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya usalama, huku operesheni za uokoaji zikiendelea katika maeneo yaliyoathirika zaidi.
Chanzo; Global Publishers