vWaziri Mkuu wa Ivory Coast Robert Beugré Mambé na serikali yake wamejiuzulu kufuatia uchaguzi wa wabunge uliofanyika Desemba 27 mwaka uliopita.
Kufuatia taarifa ya Rais Alassane Ouattara hapo jana amekubali kujiuzulu kwa mawaziri wake, ikiwemo Waziri Mkuu Mambé, licha ya chama chake cha RHDP kushinda uchaguzi huo kwa asilimia 77.
Hatua hii inakuja miezi miwili baada ya Rais Ouattara kuchaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, baada ya ushindi wa karibu asilimia 90 ya kura.
Rais Ouattara anatarajiwa kumtaja Waziri Mkuu mpya na kuwateuwa mawaziri wapya katika siku zijazo, baada ya chama chake kupata viti 198 kati ya 255 katika Bunge la Taifa.
Ripoti zinaonyesha huenda baadhi ya mawaziri waliyojiuzulu wakarejeshwai tena serikalini, kutokana na kuchaguliwa kama wabunge.
Licha ya kujiuzulu, mawaziri waliopo wameombwa kuendelea kusimamia shughuli za wizara zao hadi pale warithi wao watakapoteuliwa rasmi.
Chanzo; Crown Media