Serikali ya Marekani imeishutumu Rwanda kwa kutotekeleza kwa uaminifu makubaliano ya amani yaliyotiwa saini Washington yanayolenga kuishia machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ikisema wazi kuwa vitendo vya Kigali vimekuwa ni ukiukwaji wa makubaliano hayo yaliyofikiwa chini ya usimamizi wa Rais Donald Trump.
Msemaji wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, alisema hatua za Rwanda zinakiuka makubaliano na kwamba Washington itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinaheshimiwa.
Huu ni mwito mkali unaokuja baada ya wanamgambo wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda kuchukua udhibiti wa mji wa Uvira, hatua ambayo imeripotiwa kuleta vurugu na kusababisha mamilioni ya wakimbizi kutokana na vita mashariki mwa DRC.
Waziri Rubio ameonya kwamba endapo Rwanda itaendelea kupuuza makubaliano hayo, nchi hiyo inaweza kukabiliana na hatua kali za kidiplomasia au kijeshi zilizopo mezani, kama zile zilizopewa sifa kubwa wakati wa operesheni ya Marekani dhidi ya serikali ya Venezuela mwanzoni mwa mwaka huu tukio lililoibua mjadala mkubwa wa kimataifa.
Matamshi hayo yameibua hofu ya kuenea kwa mgogoro wa muda mrefu wa mashariki mwa DRC hadi kwenye ukanda mpana wa Afrika, na kuashiria hatari ya kuzuka kwa misukosuko kama ilivyoshuhudiwa Caracas hivi karibuni.
Chanzo; Cnn